3 research outputs found

    Umuhimu na Changamoto za TEHAMA katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili kwa Wageni

    Get PDF
    Ulimwengu wa utandawazi umesababisha kusambaa kwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), hususani matumizi ya kompyuta na viambata vyake. Kwa hali hiyo, maendeleo yamesababisha kuenea kwa lugha zinazotumika katika teknolojia hiyo kama vile Kiingereza na lugha nyingine za Kimagharibi, na kwa kiasi kidogo, lugha za Kiafrika kama vile Kiswahili. Hata hivyo, TEHAMA imekuwa ikitumiwa na walimu na wanafunzi katika kufundishia na kujifunzia lugha za kigeni hasa Kiingereza kama inavyoelezwa na Lopez (2016), Bostina (2016), Bilyalova (2016). Aidha, zipo tafiti chache zilizozungumzia changamoto za kutumia Kiswahili katika TEHAMA, kwa ujumla, bila kuzungumzia namna Kiswahili kinavyoweza kutumika kiteknolojia katika ufundishaji na ujifunzaji kwa wageni. Kwa hiyo, makala haya yamejadili suala hilo na yanajikita katika kufafanua umuhimu na changamoto za TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kwa wageni. Aidha, makala haya yametoa mapendekezo ya nini cha kufanya ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika ufundishaji na ujifunzaji huo. Data zilizotumika katika makala haya zimepatikana kwa njia ya dodoso. Mkabala wa kitaamuli umetumika katika kuchambua data. Matokeo yamebaini kuwa kuna umuhimu wa kutumia TEHAMA katika kufundishia na kujifunzia Kiswahili kwa wageni kwani inarahisisha ufundishaji kwa maana ya kutumia muda mfupi kufundisha mambo mengi. Pia, inamfanya mwanafunzi afurahie somo bila kuchoka na kupunguza gharama za ujifunzaji. Pamoja na umuhimu huo, zimebainika changamoto katika matumizi ya TEHAMA, yaani wakati mwingine wanafunzi wanapata shida kutumia matini zilizo mtandaoni kutokana na kukosa mwingiliano wa moja kwa moja na mwalimu, kukosekana kwa matini za kutosha na zilizoandikwa kwa usahihi mitandaoni, kukosekana kwa vifaa kama projekta na kompyuta na baadhi ya walimu na wanafunzi kutokuwa na maarifa ya kutosha ya matumizi ya vifaa hivyo. Kwa ujumla, makala yanahitimisha kwamba upo umuhimu wa kupendekeza mbinu zinazoweza kukabiliana na changamoto hizo kama vile kuwa na semina za mara kwa mara za kufundisha namna ya kutumia vifaa vinavyohusiana na TEHAMA, kuwa na vifaa vya kutosha na vinavyokidhi mahitaji y

    Aina za dosari za kifonolojia zinazojidhihirisha kwa wajifunzaji wa Kiswahili katika jamii ya Wamaasai

    Get PDF
    Katika taaluma ya ujifunzaji na ufundishaji wa lugha ya pili (kuanzia sasa Lg2) imethibitika pasi shaka kuwa wajifunzaji wa Lg2 ambao tayari mifumo yao ya lugha ya kwanza (kuanzia sasa Lg1) imeimarika kikamilifu miongoni mwao, hukabiliwa na ufanyaji wa dosari kila wanapojaribu kujifunza lugha nyingine ya ziada. Hali hiyo huwa ni kubwa zaidi pale ambapo mjifunzaji wa lugha ya ziada anajifunza lugha ambayo kimfumo ni tofauti na Lg1 kama ilivyo kwa wajifunzaji wa Kiswahili katika jamii ya Wamaasai. Tafiti zaidi zinaonesha kuwa  wajifunzaji wa aina hiyo hupata dosari katika viwango vyote vya lugha; yaani fonolojia, mofolojia, sintaksia, semantiki na pragmatiki (Wei, 2008) japo kwa viwango tofauti. Kadiri ya ufahamu wetu, hakuna utafiti uliofanyika wa kuchunguza aina za dosari za kifonolojia  zinazofanywa na wajifunzaji wa Kiswahili katika jamii ya Wamaasai. Ukosefu wa utafiti wa aina hiyo mbali na mambo mengine  umesababisha ukosefu wa taarifa anuwai za aina za dosari za kifonolojia zifanywazo na wajifunzaji wa lugha ya Kiswahili katika jamii ya Wamaasai. Kwa kuongozwa na Nadharia ya Usasanyuzi Dosari (Corder, 1967), makala inabainisha aina za dosari za kifonolojia  zinazojidhihirisha kwa wajifunzaji wa Kiswahili katika jamii ya Wamaasai. Utafiti ulifanyika katika kijiji cha Ilkurot na Lengijave, kwa kutumia sampuli ya wanafunzi 50 waliogawika katika makundi mawili, wanafunzi 25 kutoka shule za msingi na wanafunzi 25 kutoka shule za sekondari. Mbinu kuu ya ukusanyaji wa data ilikuwa ni uandishi wa insha na usimuliaji wa hadithi. Matokea ya utafiti yanaonesha kuwa wajifunzaji Kiswahili katika jamii ya Wamaasai hufanya aina mbalimbali za dosari za kifonolojia kama vile: dosari za udondoshaji wa fonimu, ubadilishaji wa fonimu na uchopekaji wa silabi mwanzoni na mwishoni mwa neno

    Changamoto za Istilahi katika Uandishi wa Tasinifu za Uzamili wa Kiswahili Tanzania

    No full text
    Uthabiti wa taasisi yoyote ya elimu ya juu hasa katika ngazi ya Chuo Kikuu unatokana na uimara wa programu zitolewazo katika taasisi husika na ubora wa wahitimu katika ngazi husika. Kuimarika kwa programu kama za Umahiri na Uzamivu ni sifa mojawapo ya taasisi ya elimu ya juu. Kuimarika huko hakutawezekana kama eneo la istilahi za kitaaluma zinazotumika katika uwanja husika isimu/fasihi na methodolojia ya utafiti hazitakuwa sanifu na thabiti. Hivyo, makala haya yanafafanua changamoto za kiistilahi katika pragramu za M.A. (Kiswahili) na PhD. (Kiswahili) katika TATAKI kwa uzoefu wa miaka mitano. Swali linaloibuliwa na makala haya ni: je, kutakuwa na usanifu wa programu kama usanifishaji wa istilahi haujafanywa na taasisi husika? Mwito wa makala haya kwa watawala wa TATAKI na Chuo Kikuu kwa ujumla wake, ni kwamba, hima usanifishaji wa istilahi katika Kiswahili hasa katika eneo la methodolojia ufanyike kabla ya jahazi kuzama
    corecore