1 research outputs found

    Kuchunguza Tamathali za Usemi katika Mashairi ya Magazetini: Uchunguzi kifani wa Mashairi ya UKIMWI katika Magazeti ya Kiswahili

    Get PDF
    Utafiti huu umeshughulikia matumizi ya lugha ya tamathali za usemi katika mashairi ya magazetini. Ili kukamilisha lengo hili kuu madhumuni mahususi matatu yalitimizwa. Madhumuni hayo yalihusu kubainisha tamathali za usemi, dhamira na dhima za tamathali za usemi katika kujenga dhamira mbalimbali katika mashairi ya magazetini. Mtafiti ametumia mbinu za uchambuzi wa kimaudhui, usaili na upitiaji wa nyaraka katika kukusanya data za utafiti. Mikabala ya kifasihi na ule wa kimaelezo ndio iliyotumika katika kuchambua data za utafiti wetu. Kwa ujumla utafiti umeweza kukusanya data ambazo zimeweza kujibu maswali ya utafiti wetu ambapo imethihirika kwamba, mashairi ya magazetini yamesheheni matumizi ya tamathali mbalimbali za usemi. Pia imebainika kwamba tamathali hizo za usemi zinatumika kujenga dhamira mbalimbali na mwisho tamathali za usemi zimebainika kuwa na dhima mbalimbali za kifani na kimaudhui katika kujenga na kuwasilisha dhamira mbalimbali kuhusiana na masuala ya UKIMWI kwa jamii ya Kitanzania. Mwishoni mwa utafiti kumetolewa mapendekezo kwa wadau mbalimbali wa mashairi ya magazetini kuhusiana na namna bora za kuimarisha mashairi hayo ili yaendelee kutekeleza wajibu wake kwa jamii. Pia, tumetoa mapendekezo kwa ajili ya tafiti za baadaye katika uwanja wa mashairi ya magazetini
    corecore