Upimaji wa ufahamu wa kiswahili kama lugha ya kufundishia shule za msingi

Abstract

Utafiti ulilenga kufanya upimaji wa ufahamu wa kiswahili kama lugha ya kufundishia shule za msingi kwa wanafunzi wa darasa la VII katika halmashauri ya Geita. Utafiti ulifanyika ili kutoa mchango wa kitaaluma katika lugha ya kufundishia shule za msingi kuona ufahamu walio nao wanafunzi. Lengo la utafiti ni kupima ufahamu wa wanafunzi katika lugha kiswahili kama lugha ya kufundishia shule za msingi na Malengo Mahususi yalikuwa ni kupima ubobezi wa Kiswahili kama lugha ya kufundishia kwa wanafunzi wa shule za msingi Geita na Kutathmini kiwango cha ubobezi wa kiswahili dhidi ya sifa za lugha ya kufundishia shule za msingi. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya umilisi wa mawasiliano ya Canale na Swain (1980, 1981), ili kuweza kutimiza malengo ya utafiti huu na pia kujibu maswali ya utafiti huu. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia njia ya zoezi la umilisi wa lugha, usaili, hojaji na mbinu ya usomaji wa nyaraka. Eneo la utafiti lilikuwa wilaya ya Geita, kata ya Nyakamwaga. Walengwa wa utafiti huu walikuwa ni wanafunzi wote wa darasa la saba na sampuli ya utafiti ilikuwa ni wanafunzi 20 toka shule hizo 5 ambapo jumla yake ni watafitiwa 100. Watafitiwa hao waliosailiwa na kujibu maswali ya hojaji na pia maswali ya zoezi la umilisi wa lugha. Watafitiwa waliteuliwa kwa kuzingatia kigezo cha unasibu. Uchambuzi wa data umefanyika kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na kitakwimu. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwa wanafunzi wana ujuzi na ubobezi katika lugha ya kufundishia hivyo wana ufahamu wa kutosha katika vipengele ambavyo mtafiti aliwapima katika lugha ya kiswahili kama lugha ya kufundishia shule za msingi. Ufahamu wa wanafunzi katika lugha ya Kiswahili unakidhi vigezo vyote vya kutumia lugha hiyo katika kufundishia na kujifunzia shule za msingi

Similar works

Full text

thumbnail-image

Digital Library of Open University of Tanzania

redirect
Last time updated on 10/12/2020

Having an issue?

Is data on this page outdated, violates copyrights or anything else? Report the problem now and we will take corresponding actions after reviewing your request.