Translating Culture: Literary Translations into Swahili by East African Translators.

Abstract

Lengo la makala hii ni kujaribu kufafanua jinsi wafasiri walivyotafsiri kwa Kiswahili baadhi ya riwaya zilizoandikwa kwa lugha za kigeni, enzi za baada ya nchi za Afrika kujipatia uhuru. Kwa ajili ya mada yenyewe nimechagua mkusanyo wa riwaya nne zilizotafsiriwa na Watanzania, yaani Shamba la wanyama (kilichoandikwa na Fortunatus Kawegere, 1967), Shujaa Okonkwo (Clement Ndulute, 1973), Mzee na bahari (Cyprian Tirumanywa, 1980) na Barua ndefu kama hii (Clement Maganga, 1994). Wafasiri hao walikabiliana vipi na vipengele vya kitamaduni vya lugha chanzi (za jamii zenye maisha, dini, misemo, methali tofauti na yao n.k.)? Kwa kuzingatia swali hilo, makala inaeleza baadhi ya mbinu zilizotumiwa na watafsiri wa Kiswahili wakishughulika na maandishi kutoka kwa fasihi ya kigeni

    Similar works