Mashairi ya waadhi `verses of admonition`:

Abstract

Aliyetunga kasiga hii, Sheikh Abgallah al-Husni, alikuwa ni mtu maarufu sana Mombasa .. Kwa muda wa myaka arobaini takriban alikuwa akisomesha elimu za gini, msikiti wa Anisa, Mjuwakale; piya alikuwa akitoa waadhi msikiti huu na mahali pengine .. Antunga kasiga mbili za waadhi, moja katika hizo ndiyo hii tuliyoishereheya katika makala haya .. W akati wa kutungwa waadhi huu - 1368 (mwaka 1948 wa milagi) - Mombasa ilikuwa ikali mji wa kiSawahili, yaani mji wa kilsilamu; lakini kulikuwa kuna mabadiliko makubwa yaanza, mabadiliko ambayo mwisho yanaondowa sura za uSawahili katika Mombasa na pwani nzima ya Afrika ya mashariki

    Similar works