Maelezo Kinzani ya Vipengele vya Sarufi ya Kiswahili Katika Vitabu Teule vya Shule za Upili Nchini Kenya

Abstract

Dhamira ya makala hii ilikuwa ni kuonesha tofauti za kimaelezo baina ya waandishi wa sarufi kama inavyojitokeza katika ufundishaji na ujifunzaji wa Sarufi ya Kiswahili katika shule za upili hapa nchini Kenya. Uchunguzi huu uliongozwa na Nadharia ya Sarufi Amilifu na nadharia ya Ujifunzaji Kitajiriba. Sarufi Amilifu ni ya Simon C. Dik (1978). Nadharia hii inashikilia kwamba, uzingatifu wa sarufi ya lugha unadhihirika katika utendaji wa lugha hiyo ambao unakuzwa katika matini inayoandaliwa na wataalamu wake. Nayo nadharia ya Ujifunzaji Kitajiriba iliyoasisiwa na David Allen Kolb mnamo mwaka wa 1984 inaangazia matumizi ya tajiriba katika ufundishaji na ujifunzaji. Kundi lengwa lilikuwa ni waandishi wa Sarufi ya Kiswahili, walimu wa Sarufi ya Kiswahili na wanafunzi wa kidato cha tatu. Tulitumia mbinu za usampulishaji wa kinasibu na usampulishaji wa kimakusudi kuteua sampuli iliyokusudiwa tukizingatia asilimia 30 ya jumla ya idadi lengwa. Walimu 12 na wanafunzi 120 waliteuliwa kushiriki katika uchunguzi huu. Data ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo, hojaji na mahojiano. Data katika makala hii iliwasilishwa kupitia maelezo, majedwali na asilimia. Matokeo ya makala hii yalionesha kwamba, waandishi wa Sarufi ya Kiswahili wanakinzana katika ufafanuzi wa baadhi ya vipengele vya Sarufi ya Kiswahili katika shule za upili nchini Kenya.&#x0D; Uchunguzi huu utakuwa wenye umuhimu kwa walimu wa Sarufi ya Kiswahili, wanafunzi, wataalamu wa Sarufi ya Kiswahili na wale wanaoandaa na kuchapisha vitabu vya Sarufi ya Kiswahili kwa kutambua vipengele tata katika Sarufi ya Kiswahili. Makala ilipendekeza Taasisi ya Ukuzaji wa Mitalaa ya Kenya kuvichunguza upya vitabu vya kiada na ziada vya Sarufi ya Kiswahili ambavyo vimeidhinishwa na wao huku vikiwa na tofauti za kimaelezo.</jats:p

    Similar works

    Full text

    thumbnail-image

    Available Versions