Moi University Journals
Not a member yet
331 research outputs found
Sort by
Kiswahili na Siasa: Uchanganuzi wa Ishara na Tamathali katika Tamthilia ya \u27Visiki\u27 Kisemiotiki
Makala haya yanachunguza fasihi na siasa kupitia tamthilia ya Kiswahili. Lengo kuu la makala haya ni kuchanganua ishara na maana za kisiasa na jinsi zinavyojitokeza katika tamthilia ya Visiki kwa kutumia nadharia ya semiotiki, misimbo ya Barthes ya kiseme,kiishara na matukio. Kisemiotiki, ishara huathiri namna msomaji wa matini za kifasihi huishia kufasiri maana nasibishi ya kina ya matini. Tulifasiri ishara na uashiriaji katika tamthilia ya Visiki kwa sababu kisemiotiki, lugha ya kiishara huwa na uwezo wa kuwasilisha maana mbalimbali kwa njia ya uashiriaji. Kutokana na ufasiri huo wa ishara, makala haya yanajadili kuwa, wakati umefika ambapo siasa za bara hili zinastahili kubadilika na kuzingatia demokrasia za Kiafrika, haki za wapiga kura, za kibinadamu pamoja na kukumbatia maarifa mapya ya kisasa. Makala inahitimisha kwamba, Mataifa ya Kiafrika ni sharti yazinduke kisiasa na kukomesha lawama dhidi ya mataifa ya Kimagharibi kila yanaposhindwa kudhibiti hali nchini mwao
Uanishaji wa Vigezo vya Utoaji wa Majina ya Utani kwa Walimu nchini Tanzania
Wanafunzi huwapa walimu wao majina mbalimbali ya utani kipindi wawapo shuleni. Majina hayo hurejelea sifa tofauti tofauti zinazowahusu walimu hao ama moja kwa moja au si moja kwa moja. Je kuna sababu gani za utoaji wa majina hayo ya utani? Je ni vigezo gani hutumika katika kutoa majina hayo ya utani kwa walimu? Haya yalikuwa maswali yaliyohitaji kujibiwa na makala haya. Data za utafiti zimekusanywa kupitia hojaji zilizotumwa katika makundi 3 ya WhatsApp ya wanafunzi waliohitimu elimu ya sekondari katika shule ya Star, Nyasho, na Morogoro. Matokeo yanaonesha kuwa majina ya utani hutolewa kwa kuzingatia vigezo mbalimbali. Aidha, sababu zinazochochea utoaji wa majina hayo ni mahusiano mabaya kati ya walimu na wanafunzi, walimu kutofahamika majina kwa wanafunzi wao na tofauti za uzungumzaji
Kanuni za Ubuntu katika Methali za Kiswahili
Makala haya yalichanganua kanuni za ubuntu zinazojitokeza katika methali za Kiswahili. Kanuni za ubuntu zinadhihirika katika methali sio tu za Kiswahili bali za jamii mbalimbali za Kiafrika. Waafrika walitumia vipera mbalimbali vya fasihi simulizi kuelimisha na kuadilisha wanajamii (Akaka na Wandera-Simwa, 2024). Umoja wa kijamii pamoja na maadili mengine yanayokuza na kuhimiza uhusiano mwema baina ya Waafrika unadhihirika katika fasihi simulizi zao zikiwemo methali. Maadili ya kimaisha yanayosisitiza umoja na thamani nyinginezo miongoni mwa jamii za Kiafrika zimefumbatwa katika methali zao. Maana ya dhana ubuntu inatokana na mojawapo ya methali za jamii za Kiafrika. Ubuntu kama falsafa ilianza kutumiwa katika maandishi tangu mwaka wa 1846 lakini ufafanuzi wa dhana hii unatokana na methali ya Kinguni umuntu ngumuntu ngabantu (Gade, 2011). Mtafiti aliteua kimaksudi kamusi za methali za Wamitila (2001), King’ei na Ndalu (1989) na Omusikoyo (2021) ili kuchanganua kanuni za ubuntu zilizomo katika baadhi ya methali. Methali zilizo na kanuni za ubuntu ziliteuliwa kimakusudi. Kanuni za ubuntu zilizomo zikatambuliwa na kujadiliwa vile zinavyojitokeza katika methali za Kiswahili. Nadharia ya uchanganuzi hakiki wa diskosi kwa mujibu wa Fairclough (1992) iliongoza utafiti huu. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa methali za Kiswahili zimesheheni kanuni za ubuntu zinazozikumbusha jamii za Kiafrika kushirikiana, kupendana na kujaliana
Changamoto katika Kutafsiri Matini za Kisayansi
Makala haya yanajadili kuhusu changamoto zinazojitokeza wakati wa kutafsiri matini za kisayansi na mbinu za kukabiliana na changamoto hizo. Tafsiri ya matini za kisayansi, kwa mujibu wa Ghazala (1995), inahusu kufasiri maneno, hasa katika uga wa sayansi na tekinolojia wa aina zote, kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine. Kutokana na maendeleo ya sayansi na tekinolojia, ni dhahiri kwamba tafsiri katika uga huu haiwezi kuepukika. Hata hivyo, kwa mujibu wa Mwansoko na wenzake (2006), tafsiri ya kisayansi ni miongoni mwa tafsiri ngumu kulinganisha na tafsiri nyingine. Kwa hivyo, makala haya yamechunguza changamoto zinazosababisha ugumu huo na namna ya kukabiliana nao. Data za utafiti zimepatikana kwa njia ya dodoso na kuchanganuliwa kwa kuongozwa na Nadharia ya Aina ya Matini iliyoasisiwa na Reiss miaka ya 1970. Aidha, matokeo ya utafiti yamebaini kwamba changamoto za kutafsiri matini za kisayansi zinasababishwa na mambo yafuatayo: uvumbuzi wa kisayansi, ugumu wa istilahi katika matini za kisayansi, kukosekana kwa visawe vya moja kwa moja katika lugha lengwa, uchache wa vifaa na ukubwa wa gharama za vifaa vya tafsiri na mfumuko wa istilahi mbalimbali zinazorejelea dhana moja. Kadhalika, utafiti umebaini kwamba zipo mbinu zinazoweza kutumika kukabiliana na changamoto hizo kama vile; uundaji wa maneno mapya, ufafanuzi, kununua vifaa bora vya tafsiri na wataalamu kukubaliana na kuchagua istilahi zinazofaa zaidi
Mikakati ambayo Wanaume Wanatumia katika Harakati za Kupigania Ukombozi Wao katika Riwaya Teule za Kiswahili: \u27Njozi Yapata Mtenzi\u27 na \u27Nguu za Jadi\u27
Makala haya yanachunguza mikakati ambayo wanaume wametumia katika harakati za kupigania ukombozi wao. Jinsia ya kiume imeteuliwa kimaksudi kutoka riwaya teule za Kiswahili Njozi Yapata Mtenzi (2018) na Nguu za Jadi (2019). Makala haya yameegemea Nadharia ya Uwezo-Mkuu wa Kiume. Kazi hii itasaidia kupiga msasa harakati za kuwakomboa wanaume kutoka makundi ya watu kandamizi na athari za ukandamizaji. Kadhalika, ukombozi huu unaweza kuwa wa kifikra, kiuchumi, kidini na hata kiutamaduni. Hata hivyo, bila kuwabadilisha wanaume na wanawake, mabadiliko ya kumkomboa mwanaume wa kisasa hayatapatikana kwa ukamilifu. Ni muhimu kuwa nafasi mpya na majukumu mapya ya wanawake yaende sambamba na nafasi mpya na majukumu mapya ya wanaume ili ukandamizaji wa jinsia ya kiume upunguzwe
Uchunguzi wa Sababu za Mtumizi ya Lakabu za Wanafunzi katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Kigeni Nchini Tanzania
Miongoni mwa maeneo ambayo lakabu hutumika ni katika ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya kigeni. Tafiti mbalimbali zimefanyika kuhusu matumizi ya lakabu katika ufundishaji na ujifunzaji wa Lgn na kubainisha sababu mbalimbali za kutumia lakabu katika ufundishaji wa lugha kwa ujumla. Licha ya kubainisha sababu hizo, tafiti hizo ziliangazia lugha mbalimbali bila kuangazia sababu za matumizi ya lakabu za wanafunzi katika ufundishaji na ujifunzaji wa Lgn mahususi. Makala haya yameshughulikia sababu za matumizi ya lakabu za wanafunzi katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama Lgn nchini Tanzania. Data za utafiti huu zimekusanywa kutoka kwa walimu 6 wanaofundisha Kiswahili kama Lgn na wanafunzi 15 kutoka katika vyuo/taasisi 03 nchini Tanzania ambazo ni Taasisi ya Kiswahili na Utamaduni (KIU), Chuo cha Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa (MS TCDC) na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA). Data zimekusanywa kwa mbinu ya usaili na kuwasilishwa kimaudhui kisha zikatolewa maelezo yaliyoongozwa na Modeli ya Elimu ya Kijamii ya Robert C. Gardner, 2005. Sababu zilizobainika katika matokeo hayo ni pamoja na kuwapa wanafunzi utambulisho, kupata urahisi wa kuwakumbuka wanafunzi kwa lakabu zao, kuchochea motisha ya wanafunzi katika ujifunzaji wa Kiswahili kama Lgn, kurahisisha ufundishaji wa sarufi, kukidhi kipengele cha kiutamaduni, kuepuka makosa ya matamshi ya majina ya wanafunzi na kutumia lakabu kwa sababu tu ni utaratibu wa chuo/taasisi husika. Makala haya yanapendekeza kuwapa walimu mafunzo kuhusu matumizi ya lakabu ili watambue faida zake katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama Lgn. Pia, wito unatolewa na makala haya kwa wataalamu wengine kuchunguza madhara ya kutumia lakabu zisizofaa katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni ili waweke bayana maarifa hayo
The Role of Tour Operators’ Sustainable Environmental Practices on Visitor Choice Behavior in Narok County, Kenya
In Narok County, which hosts the Maasai Mara National Reserve, tourism is a major earner important for Kenya’s economy overall. Nonetheless, the rise in tourism operations in this ecologically sensitive area has caused environmental degradation, endangering the sustainability of the region\u27s natural heritage. Narok County is thus the epicenter of this study. The objective of this study is to examine the contribution of tour operators\u27 sustainable environmental practices on the choice behavior of the visitors. The research design used was mixed method research design. The target population was 314 tour operators and sample population were 176 tour operators that are registered by Tourism Regulatory Authority, are member of Kenya Association of Tour Operators and have access to Narok county. The target population of visitors were 76,217 and sample population was 397 visitors visiting attractions in Narok County. simple random sampling technique was employed to select the tour operators and visitors. Questionnaires were issued to visitors and tour operator staff to collect primary data. Interviews schedules and observation checklist were used to get information from high ranking official of tour operators. Data was analysed using statistical package for social science SPSS software version 20.0. The value of R square was 0.259, an indication that 25.9 percent of visitor choice behavior is caused by tour operators’ sustainable environmental practices. The coefficient of tour operators’ sustainable environmental practices had a positive and statistically significant effect on visitor choice behavior (β=0.557, P<0.05). The beta estimate suggests that a unit change in tour operators’ sustainable environmental practices result to 0.557 units change in visitor choice behavior in Narok County, Kenya. The outcomes of the study lead the to the conclusion that the sustainable environmental practices of tour operators have an impact on the decision-making behavior of visitors. The study recommends for the need of the government to actively involve tour operators in key decisions regarding achieving sustainable tourism in destinations
Matumizi ya Usambamba kama Nduni ya Kimtindo katika Kuibua Maudhui ya Dini katika Riwaya ya \u27Paradiso\u27
Makala haya yanachunguza matumizi ya usambamba kama nduni ya kimtindo katika kuibua maudhui ya dini katika riwaya ya Paradiso. Tunachunguza miundo mbalimbali ya kiusambamba iliyotumika katika riwaya hiyo kuibua maudhui ya dini. Suala la dini ni la msingi katika jamii mbalimbali kwa vile dini imeshikamana na maisha ya kawaida ya wanajamii. Ndani ya mada ya jumla ya dini, riwaya hii inaangazia dhamira zinazoathiri jamii kama vile ufisadi na ujilimbikiziaji mali, ufungamano wa siasa na dini, pamoja na masuala ya kijinsia. Tulidondoa vifungu kutoka katika riwaya hiyo kwa mkono kwa sababu haipatikani kielektroniki. Data iliteuliwa kimaksudi kwa kulenga maudhui yanayohusu suala la dini. Katika ukusanyaji na uchambuzi wa data tumetumia Nadharia ya Uchimuzi. Orodha ya kategoria za kiisimu na kimtindo ya Leech na Short (2007) ilitumiwa kubainisha ngazi kuu za uchunguzi wa kimtindo. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kwamba usambamba ni njia kuu aliyoitumia mwandishi kuibulia na kusisitizia maudhui kuhusu dini. Usambamba huu unajitokeza katika ngazi za virai na vishazi na unahusisha aina mbalimbali kama vile anafora, epifora, tanakuzi na mjalizo. Usambamba wa aina ya anafora ndio umedhihirika zaidi katika riwaya ya Paradiso. Makala haya yanapendekeza kwamba usambamba wa kisintaksia unafaa kuhusianishwa na usambamba wa kileksika katika kuzichambua kazi za kifasihi za Kiswahili kimtindo
Athari ya Mielekeo ya Walimu wa Shule za Msingi kuhusu Ufundishaji wa Kiswahili na Mazoezi Yake katika Mtaala wa Umilisi
Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mielekeo ya walimu huwa na athari miongoni mwa wanafunzi. Sababu ni kuwa wanatangana nao kwa asilimia kubwa ya muda. Makala haya yanajadili athari ya mielekeo ya walimu kuhusu ufundishaji wa Kiswahili na mazoezi yake katika Mtaala wa Umilisi kwa kujikita kwenye Gatuzi dogo la Masaba Kusini. Mtaala wa Umilisi umechukua nafasi ya Mtaala wa 8-4-4 ambao umekuwa ukitumika nchini Kenya kwa zaidi ya miongo mitatu. Mtaala wa Umilisi kwani unasisitiza utendaji wa yale mwanafunzi amefundishwa ili kuboresha umilisi wake na kuwa na ujuzi wa kutumia maarifa aliyopata katika maisha yake ya kila siku. Makala haya yanatalii namna mielekeo ya walimu kuhusu ufundishaji wa Kiswahili imeweza kuathiri wanafunzi. Nadharia ya Vitendo Vilivyofikiriwa ilizingatiwa katika makala haya. Data ilikusanywa miongoni mwa wasailiwa kwa kutumia mijadala ya makundi madogo ya wanafunzi kumi kutoka gredi ya kwanza hadi tatu kutoka shule kumi ambazo ziliteuliwa kimaksudi. Pia, wasailiwa waliteuliwa kimaksudi. Waliulizwa maswali na majibu yalinakiliwa na kurekodiwa na mtafiti akisaidiwa na walimu wao kwa sababu walikuwa wachanga. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa na kuwasilishwa kupitia majedwali ambayo yalijadiliwa kwa kina. Makala haya ni muhimu kwani itawasaidia walimu kujua zaidi athari waliyo nayo kwa wanafunzi na itasaidia katika kuboresha utekelezaji wa kina na ufundishaji bora wa Kiswahili katika Mtaala wa Umilisi
Perceived Role of Local Stakeholders’ Networks on Sustainable Tourism Development in Selected Group Ranches in Amboseli Ecosystem, Kajiado County, Kenya
Sustainable Tourism Development (STD) has emerged due to the exponential growth of tourism, which has significantly impacted natural and socio-cultural resources. The need for sustainability, as highlighted in literature like the Brundtland Report, is critical. It is a general consensus that scarcity of resources is a problem facing tourism organizations the problem and this has prompted local businessmen to source for external resources in their networks. This corroborates the fact that networks present an important source of support for businesses. This study focused on the role of stakeholders’ networks in promoting sustainable tourism in the Amboseli Ecosystem, Kajiado County. A notable gap exists in information sharing and stakeholder networking, with existing frameworks primarily centered on conservation rather than STD. Stakeholders, including accommodation providers, local destination organizations, local communities, conservation organizations, the government, and travel organizers, play a crucial role in ensuring the longevity of sustainability initiatives. Networking offers solutions to industry challenges by fostering unified decision-making and addressing local resource and expertise deficiencies The study employed descriptive and explanatory research designs, targeting a sample population of 420 participants from different groups in the Amboseli ecosystem, including community members, lodge managers, Kenya Wildlife Service officials, and NGO representatives. Data were collected using questionnaires and structured interviews, analyzed through Pearson and Regression Analysis. Results showed that stakeholder networks significantly and positively influence sustainable tourism development (r=0.246, p=0.000). Collaborations among stakeholders and existence of community mobilization initiatives were proved to be an important component in fostering stakeholders’ networks in AE. The study recommendations include fostering stakeholder networks, capacity building for leaders, enacting legislation to involve local communities, forming societies for local tourism entrepreneurs to network, and collaborating with local universities and research institutions on sustainable tourism issues