191 research outputs found

    Kuchunguza Dhamira za Nyimbo za Uganga Katika Jamii za Waswahili Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba

    Get PDF
    Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza dhamira za nyimbo za Uganga katika jammi za waswahili Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba. Ili kutimiza lengo hili kuu tulikuwa na madhumuni mahususi matatu ambayo ni kubainisha dhamira zinazopatikana katika nyimbo za uganga, kufafanua undani wa dhamira za nyimbo za uganga zilimo katika jamii ya watu wa Kusini Pemba na kufafanua vipengele vya kifani vinavyosaidia kuibua dhamira zinazojitokeza katika nyimbo za uganga. Data za utafiti zimekusanywa kwa kutumia njia ya usaili na njia shirikishi katika maskanini. Data hizo zilikusanywa na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Vile vile njia za kimaktaba zilitumika kwa mtafiti kwa ajili ya kujisomea kazi tangulizi na maandiko tafauti kwa lengo la kujiongezea maarifa na kufanikisha utafiti wake. Pia uchambuzi wa data ulifanywa kwa kutumia mkabala wa kinadharia. Nadharia zilizotumika ni Simiotiki na Mwitiko wa Msomaji. Ama kuhusu matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kwenye nyimbo za uganga kuna siri ambazo zimejificha na zilihitajika kuwekwa bayana na mtafiti. Kwa upande wa dhamira zilizojitokeza katika nyimbo za uganga zilitoa dhamira kama vile suala la Mmongonyoko wa Maadili, umoja na mshikamano, malezi, matabaka na kadhalika. Mwisho matfiti alitoa hitimisho, mapendekezo ya tafiti nyingine zifanyika katika muktadha wa uganga kwa kuangalia misamiati na njungu katika tiba ya uganga na kuiomba jamii yake iziendeleze tiba za asili katika fani ya uganga

    Athari ya Mazingira Asilia ya Mtunzi katika Matumizi ya Kujibadilisha Kimazingaombwe: Uchunguzi wa Riwaya Teule za S. Robert na E. Kezilahabi

    Get PDF
    Makala haya yalikusudia kuchunguza athari ya mazingira asilia ya mtunzi katika matumizi ya kujibadilisha kimazingaombwe. Ili kulifikia lengo hilo, makala yameangazia jinsi mazingira asilia ya watunzi wawili yaani, Shaaban Robert na Euphrase Kezilahabi yalivyoathiri suala la matumizi ya mbinu ya kujibadilisha kimazingaombwe. Kazi za Shaaban Robert zilizoteuliwa ni riwaya za Adili na Nduguze (1952) na Kufikirika (1946) na kazi za Euphrase Kezilahabi zilijumuisha riwaya za Nagona (1990) na Mzingile (1991). Kujibadilisha kimazingaombwe ni mbinu ya kisanaa inayoonekana kuwa mashuhuri katika kazi za kifasihi za mihula mbalimbali. Mathalani, mbinu hii inapatikana siyo tu katika kazi za kifasihi zilizojitokeza katika kipindi cha usasabaadaye, bali pia mbinu hii inaonekana hata kwenye kazi za kale zaidi, hususani kipindi cha kabla ya usasabaadaye. Kutokana na usuli huo, riwaya za Shaaban Robert zilizoteuliwa zimewakilisha kipindi kabla ya usasabaadaye ilhali riwaya za Kezilahabi ni za kipindi cha usasa na usasabaadaye. Tumechagua riwaya zilizoandikwa katika vipindi hivyo tofauti ili kuthibitisha kuwa mbinu ya kujibadilisha kimazingaombwe ni ya kale, ilikuwako hata kabla ya kipindi cha usasabaadaye. Matokeo yanaonesha kwamba tafsiri ya dhana au wazo katika kazi ya kifasihi imefungamana mno na muktadha wa kijamii uliozaa kazi hiyo. Kutokana na athari ya muktadha wa kijamii, dhana, wazo, suala au tukio fulani linaweza kuonekana la kimazingaombwe katika kazi ya kipindi fulani ilhali dhana, wazo, suala au tukio hilohilo linaweza kuonekana kuwa la kawaida (lisilo la kimazingaombwe). Mabadiliko hayo yanaweza kusababishwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia au na maingiliano ya jamii kiutamaduni na kiimani. Kwa kuongozwa na mtazamo huu, kujibadilisha kimazingaombwe kumebainishwa katika riwaya teule na kisha imeelezwa jinsi ujitokezaji wa mbinu hii ulivyofungamana na uhalisia wa maisha ya wanajamii kadiri ya mazingira asilia yaliyowazaa, kuwalea na kuwakuza watunzi wa riwaya teule

    Utendaji wa Uganga wa Pepo Zanzibar

    Get PDF
    研究ノート・資

    Baroja en África: En torno a Paradox, rey

    Get PDF

    Realms unseen: Albinism and epistemic decoloniality in tanzania

    Get PDF

    英文要旨

    Get PDF

    They bewitched the generator: state power and religious authority at the New Year’s festival in Makunduchi, Zanzibar

    Get PDF
    The New Year’s festival in Makunduchi, Zanzibar, has been one of the central sites for the interaction between state power and religious authority. It has changed considerably since colonial times, as political rituals were grafted onto religious ones, and a commercial fair developed. In this article, it is argued that these changes can be explained in part by the renegotiation, both in conflict and co-operation, of the relationship between local religious experts and state officials. First the New Year’s rituals as central practices for the production of local religious authority is analysed. Then the colonial history of the festival is discussed, before finally turning to the interactions between state power and local authority at the festival in post-colonial times
    corecore